July 6 mwaka huu FDA (food and drug administration), U.S.A, wamepitisha dawa aina ya Tenofovir/emtrcitabine yenye jina la biashara TRUVADA kama dawa ya kupunguza uhatarishi wa maambukizi ya ukimwi.(PRE-EXPOSURE PROPHYLAXIS)
TRUVADA hunywewa kidonge kimoja mara moja kwa siku kwa wale tu ambao ambao hawana virus vya ukimwi (HIV NEGATIVE), na hii itapunguza hatari ya wao kupata virusi vya ukimwi hata wakijamiiana na mwenye virusi vya ukimwi. Aina hii ya unywaji hauruhusiwi kutumiwa kwa wale ambao tayari wanamaambukizi ya ukimwi(HIV POSITIVE) kwani kwa kufanya hivyo virusi vitajenga usugu wa dawa amboa utasumbua katika matibabu yake ya kupunguza makali ya virusi.
dawa hii pia hutumika kwa pamoja(in combination) na dawa zingine katika kupunguza makali ya ukimwi.
Kwenye mkutano wa 19 wa kimataifa wa UKIMWI wa kimataifa uliofanyika Washngton DC July mwaka huu iliagizwa kuwa dawa hii ianze kutumika duniani kote ndani ya miezi 3 ijayo hasa wakisisitiza upatikanaji wa dawa hii kwa nchi zinazoendelea ikiwemo TANZANIA.
pamoja na matumizi ya dawa hii ya kupunguza hatari ya kupata virus vya ukimwi lakini bado haizuii UKIMWI kwa aslimia 100. hivyo bado inashauriwa kuendelea kujilinda na maambukizi ya ukimwi kama matumizi ya kondom n.k
source TRUVADA.COM
No comments:
Post a Comment