Utafiti huo ulionyesha kati ya wanaume 221 waliopimwa, asilimia 30.03 walikuwa na mbegu dhaifu na asilimia 17.02 walikuwa hawana kabisa mbegu zenye uwezo wa kutungisha mimba, zaidi ya maji tu....
... “Nasisitiza kuwa, pengine mwanaume aliwahi kupata watoto hapo awali, lakini sasa hivi hapati, bado atakuwa mgumba,” alisema Dk Mwakyoma...
.....Sababu za ugumba
Mwakyoma alitaja sababu za ugumba kwa wanaume kuwa ni uambukizo katika tezi inayozalisha manii.Alitaja sababu nyingine kuwa ni kemikali zinazoingia katika miili yetu, mionzi na wakati mwingine ajali inapoathiri tezi hiyo.
Dk Mwakyoma aliongeza kuwa, wanaoathirika zaidi ni wanaofanya kazi migodini, jeshini au wanaozungukwa na kemikali kwa muda mrefu.“Sababu nyingine ni joto kuzidi katika sehemu za siri za mwanaume, kubeba laptop, unene kupita kiasi na mazingira,”...
.....Shirika la Afya duniani (WHO) linathibitisha kuwa, ujazo wa manii anaopaswa kuwa nao mwanaume ili aweze kutungisha mimba ni milligram moja na nusu hadi nne na nusu na kuongeza, “Ujazo wa manii ukipungua au ukizidi basi mbegu hizo zina matatizo” alisema Dk Mwakyoma.
Utafiti uliofanywa na WHO mwaka 2009 duniani, ulibainisha kuwa, mwanaume mmoja kati ya saba wanaofika kupima afya ya uzazi hugundulika na matatizo ya ugumba.
SOURCE: gazeti la MWANANCHI february 9, 2012
No comments:
Post a Comment