WANASAYANSI
mbalimbali wanaoendesha tafiti mbalimbali za kutafuta tiba na chanjo ya
Ukimwi, wameitangazia dunia kuwa hatua waliyofikia sasa wanauona
ugonjwa huo ‘siyo hatari tena’ kwa sababu wanazo silaha zote za kuweza
kukabiliana nao.
Ila wakasema, kinachowakwamisha ni ukosefu wa fedha ambazo zinahitajika
katika kuendeleza tafiti na kuweka sera mpya za kukabili Virusi Vya
Ukimwi (VVU) duniani.
Hayo yalibainika kwenye siku ya pili ya Mkutano wa 19 wa Kimataifa wa
Ukimwi unaofanyika mjini Washington DC, Marekani na unahudhuriwa na watu
zaidi 22,000 miongoni mwao wakiwamo wataalamu wa afya, watunga sera na
wadau wa mapambano dhidi ya ugonjwa huo toka karibu kila kona ya dunia...
..... “Kwa sasa tunazo silaha zote za kisayansi kumalizia mbali gonjwa hili la
Ukimwi. Kilichobaki ni kutumia kikamilifu utaalamu huu katika fursa hii
tuliyo nayo,” alisema Rais wa Taasisi ya Kijamii ya Kimataifa ya
Mapambano dhidi ya VVU (IAS), Dk Elly Katabira...
.... Kauli ya wanasayansi hao imekuja baada ya miaka 30 ya kipindi kigumu cha
kutafiti namna ya kupata chanjo au tiba ya ugonjwa huo ambao umeua
mamilioni ya watu duniani, hususan wataalamu na nguvu kazi inayohitajika
kuimarisha uchumi...
... Licha ya tafiti mbalimbali kuonyesha kuwa kuna kila dalili ya
kupatikana kwa chanjo, miaka michache iliyopita, waligundua moja ya dawa
zinazotumika kupunguza makali ya VVU (ARV) ijulikanayo kama Truvada,
yenye uwezo wa kumkinga mwathirika kumwambukiza mpenzi wanayeshiriki
naye tendo la ndoa.
Wiki chache zilizopita,
Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA) iliidhinisha Truvada,
ambayo ilianza kutumika sehemu mbalimbali duniani tangu mwaka 2004, kuwa
ni tiba ya kuzuia kuenea kwa Virusi Vya Ukimwi (VVU).
Kwa
mujibu wa maelezo ya FDA, mwathirika anayetumia dawa hiyo anaweza
kujamiiana na mwenza wake ambaye hana VVU bila kutumia kondomu na
hatomwambukiza.
Matokeo ya utafiti huo wa ARV
yaliwahi kuchapishwa kwenye gazeti hili toleo la Februari 12, mwaka huu.
Kwa mujibu wa FDA, Truvada inatarajia kuanza kutumika na kusambazwa
duniani katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.
source GAZETI MWANANCHI
No comments:
Post a Comment