Saturday, 8 September 2012
TAHADHARI KWA WANAWAKE MNAOSAFISHWA KUCHA
siku za hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la vijana wanofanya kazi ya kusafisha na kupaka rangi kucha, vijana hawa wamebuni njia ya kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao na wameweza kupata soko kubwa sana la akinamama na mabinti wanaotaka kucha zao ziwe na mwonekan mzuri. ukitembea maeneo ya stand ya mabasi ya mwenge utapata picha ya ninachotaka kuzungumza
lakini kwa uchunguzi mdogo tu nikagundua kuwa vjana hawa hutumia vifaa vyenye ncha kali kutoa uchafu uliojishikiza chini au pembeni ya kucha, hapo ndipo nikavutiwa zaidi kuendelea kufanya kautafiti zaidi ili kujua usalama wa wateja wa huduma hii umekaaje..
nilichogundua kwa haraka ni kwamba wengi wa vijana hawa hawana DISINFECTANTS wala STERILIZER.
sasa AFYA NZURI BLOGSPOT inatoa tahadhari kwa watumiaji wote wa huduma hii kuwa wawe makini kwakuwa ni rahisi sana kupata maambikizi ya magonjwa mbalimbali katika mzingira haya.(magonjwa ya ngozi na hata VVU)
pia AFYA NZURI BLOGSPOT inawaomba watoa huduma hii kuboresha mazingira ili kuhakikisha wanalinda usalama wa afya kwa wateja wao.
vile vile tunatoa ushauri kuwa kazi za kusafisha kucha zinaweza kumalizwa na akina mama wenyewe majumbani kwao, click hapa www.wikihow.com/Clean-Your-Fingernails kupata maelezo ya jinsi unavyoweza kusafisha kucha zako wewe mwenyewe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment