Thursday, 22 December 2011

MIAKA 50 NA MAENDELEO YA AFYA

Ni miaka 50 sasa tangu tanganyika ilipopata uhuru wake kutoka Kwa wakolini wa kiingereza na tangu hapo baba wa taifa akatangaza maadui watatu MARADHI, UJINGA NA UMASKINI. Baba wa taifa aliyasema hayo akiamini kabisa taifa lililoendelea linapimwa Kwa vitu hivyo vitatu, yani huduma bora za afya, uelewa mzuri Kwa wanainchi jinsi ya kujikinga na maradhi mbalimbali hii inajenga taifa lenye afya na nguvu. Taifa lisilokua na wajinga ni taifa bora zaidi kwani wasomi hutumia uwezo wao wa kielimu kubuni na na kutengeza mbinu za kuendeleza taifa na mwisho taifa lililoendelea ni taifa linye wanainchi wenye kipato kizuri cha kuwafanya waishi maisha bora.

Kutokana na jukumu la blog yetu nilikua naomba tujadili hili la MARADHI. Wakati tanganyika inapata uhuru wake(1961) kulikua na jumla ya hospitali 100, madaktari 415 na kati ya hao wazawa walikua 12 tu.

Kwa takwimu za  mwaka 2010 ratio ya daktari kwa wananchi ni 1:20408

sasa wadau Kwa takwimu hizi zinaonyesha jins taifa hili lilivyo na changamoto kubwa katika swala zima la afya haswa ikikadiriwa Kua idadi ya watanzania inakaribia milioni 45.

pamoja na matatizo yanayowakuta madaktari na manesi ni ukweli usiopingika kuwa wamefanya kazi kubwa sana katika kipindi cha miaka hii 50. WANASTAHILI PONGEZI. Je wafanyakazi hawa wanathaminiwa kutokana kazi wanayoifanyia hii nchi?

lakini sasa wadau tujiulize je? maendeleo yaliyopatikana katika sekta hii ya afya katika kipindi hiki ndio tuliyostahili au tulitakiwa kuwa zaidi ya hapa tulipo? wadau Je?  ubora na wingi wa hospitali tulizonazo unakudhi mahitaji ya watanzania? je? ni kweli elimu ya kutosha inatolewa kwa wananchi juu ya mambo ya mbalimbali ya afya.?

miaka 50 imeshapita, Je, ni nini kifanyike kupaweka sawa pale tunaposema hapoko sawa, ili ikifika miaka hamsini ijayo tusizungumze tena kuhusu matatizo tuliyoyapata kaitika kipindi cha miaka hii 50 ya mwanzo ya uhuru wetu..?

3 comments:

  1. Nionavyo mimi miaka hii hamsini bado hali ya afya kwa wananchi ni mbaya, pamoja na ongezeko lililopo la Hospitali za Rufaa, Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati, wataalamu ni tatizo kubwa sana idadi ya madaktari,wafamasia na manesi hairidhishi. Serikali haina budi kuhakikisha kwamba wataalamu wanapatikana ili kukidhi mahitaji, ili ifikapo miaka hamsini mingine uwiano uwe angalau 1:5,000. Aidha vitendea kazi yaani vifaa mbalimbali pamoja na madawa vipewe kipaumbele pia, ili kuwezesha wananchi kupata huduma stahili.

    ReplyDelete
  2. Yaani miaka hii hamsini kwa sekta ya afya ni sawasawa na hakuna tofauti yoyote kubwa. Wananchi bado wanakabiliwa na tatizo la matibabu hasa vijijini na mijini kwa wasio na uwezo. Maana siku hizi bila pesa basi mgonjwa anaweza kufa tu kila kitu fedha. Afadhali zamani Hospitali za Misheni zilikuwa zinasaidia sana kutibu wasiojiweza bure. Lakini sasa je? Serikali ijitahidi kuondoa tatizo hili.

    ReplyDelete
  3. Uhuru na maendeleo.maendeleo bila miundombinu?.
    Tofauti ya kipato walionacho na wasionacho inaongezeka.
    Angalia uzalendo umepungua sana,kwanini?.uongozi mbovu unachangia,angalia:Kipindi cha ujamaa tunashuhudia picha za zamani watu wakilima kwa dibii na kwa pamoja,kwanini ilikuwa hivyo?watu walikuwa wanaona viongozi wao wanawajibika na hawana tofauti kubwa na wao.leo je?,umfanyishe nani kazi ya kulima au yoyote ya kujenga taifa hli ya kuwa jasho lao linaliwa na wachache?.viongozi wanaendelea kutoka vitambi,posho zinaongezeka,anasa zinazidi.

    ReplyDelete