Saturday, 3 December 2011

Matatizo ya kuoza meno


Jamani wadau hembu tuulizanena Kwa kuanza kujiuliza wewe mwenyewe, hv ni Nani Kati yatu hana tatizo la meno? Fikiria ni watu wangapi(marafiki au ndugu) unaowajua kua wanamatatizo ya meno? yawezekana pia hivi karibuni hujasikia mtu akilalamika kuhusu matatizo ya meno, mdau hii haina maana Kua tatizo hili ni dogo, hili ni kubwa liko. Pengine hujasikia kwasababu watanzania tumekua na tatizo la kupuuzia maumivu madogomadogo..sasa mdau ulitaka kujua kua taizo hili ni kubwa fanya kautafiti kadogo, uliza watu 10 maswali yafuatayo;
1. umeshawahi kun'goa jino?
2. umeshawahi kupata maumivu ya jino?
3. je sasa hivi hauna jino lililooza?
Mdau majibu utakayopata yatakushangaza na utajua tatizo hili ni kubwa kiasi gani na ningependa wadau tuweke majibu yetu kwenye comments.

Wadau tatizo hili husababishwa na wadudu (germs) ambao wanapatikana katika utando mlaini na mwembamba unaojitengeneza mara Kwa Mara kuzunguka meno kutokana sanasana na vyakula tunavyokula. Wadudu hawa hutoa kemikali Kama acid na vimeng'enyo(enzyme) hivi ndio vitu vinavyofanya jino lioze,

Jinsi ya kujikinga ni kufanya vizuri usafi wameno na usafi huu upo wa aina mbili.
Njia ya Kwanza usafi wa kila siku: usafi huu hushauriwa kufanyika si chini ya Mara mbili Kwa siku yan asubuhi baada ya kuamka na usiku kabla ya kulala Inapendekezwa kufanyika hivi kwasababu ndani ya masaa 12 wale wadudu wanaoozesha meno wanakua hawajazaliana Kwa wingi kiasi cha kuleta madhara. Na unapopiga mswaki utumie dawa ya meno.

Aina ya pili ya usafi wa meno ni ile inayofanyika Mara moja Kwa mwaka, aina hii ya usafi hufanywa na wataalamu(dental specialist). Unajua mate yetu yana madini ya calcium, madini haya hulikusanya na kuganda taratibu kwenye meno na kuweka kitu kama magamba(scale) madogomadogo, sasa chini ya magamba haya wadudu hupata nafasi ya kukaa na kuzaliana, tatizo linakuja kwamba wadudu walioko maeneo haya hawawezi kuondolewa Kwa mswaki wa kawaida.
Haya ndo mambo ambayo yanaweza kutusaidia kupunguza matatizo haya ya uozaji wa meno

Wadau tuchangie chochote ambacho unahisi kinaweza kutusaidia katika kupunguza tatizo hili.

5 comments:

  1. Kusema la ukweli hili si tatizo dogo. Hivyo basi kama jamii hatunabudi kulitilia mkazo tena kwa makini mengi. Napenda kuchangia katika hili la dawa za meno tunazotumia. Hapa Tanzania tunazo dawa za aina nyingi kama;whtedent,colgate,rungudent na nyinginezo nyingi zikiwemo za kichina. Wengi wetu tunachagua dawa ya kutumia kwa kuangalia aidha kiwango cha bei ya dawa husika au kutokana na umaarufu wa dawa husika. Ndugu zangu, nafahamu ya kuwa kutokana na hali duni ya kiuchumi kunaweza kukamfanya mtu akatumia dawa fulani kwasababu ndiyo anayoweza kuinunua. Lakini pia wapo ambao wanauwezo mzuri kiuchumi lakini wanashidwa kuchagua dawa bora ya kununua kutokana na kutofahamu dawa bora ya kulinda meno. Kusema la ukweli si kila dawa ya meno ni bora na pia ubora wa dawa haupimwi kwa kiwango cha bei ya dawa husika. Sasa swali ni kwamba, Je, dawa bora ya meno ni ipi? kwa mtazamo wangu jibu ni hili, ubora wa dawa ya meno unategemea na viundaji vya dawa husika vikiwa na malengo ya kulinda meno na kufanya meno kuwa katika hali ya usalama wakati wote. Kwa kuzingatia hili tunaweza kusema dawa fulani ni dawa bora kwa ulinzi wa meno yetu. Kwa mfano hembu fikiria kuhusu asali ambavyo huweza kudumu kwa muda mrefu bila ya kuharibika na si kwa kutumia kemikali za viwandani. Je, kwa mtazamo huu kama kukiwa na dawa yenye kitu kinacholinda asali hivi meno yetu hayatoweza kuwa na ulinzi bora na kuifanya dawa hiyo kuwa bora zaidi? Ni matumaini yangu dawa bora zipo ila inaweza kuwa ni kutona na ukosefu wa taarifa,maarifa au hali duni za kimaisha, ndizo zinazopelekea jamii kutumia dawa zisizofaa kwa ulinzi wa meno. Wito wangu kwenu ni vyema tukazingatia ubora wa dawa za meno tunazotumia hata kama ni za mitishamba.

    ReplyDelete
  2. Wadau kusema ukweli watanzania wengi wana matatizo ya meno. Ila wanakua hawajali kujilinda kama tunavyoshauriwa na madaktari wetu. Ukiwauliza wengine watakuambia ahaa! Sina fedha za kunua dawa ya meno au kwa ajili ya kumuona daktari kufanyiwa usafi wa mwaka. Jamani afya ni bora kuliko kitu kingine. Nashauri tujitahidi hata kwa kutenga fedha kidogo kidogo ili zipatikane za kufanya usafi huo wa mara moja kwa mwaka.

    ReplyDelete
  3. Wadau mbona kimya? Jamani waswahili wanasema eti dawa ya jino ni kung'oa, nami naafikiana nao kwani kwa jino lililotoboka ukiziba baada ya muda risasi inatoka na mauvimu yanabaki palepale. Wadau mnasemaje? Madaktari hebu toeni ushauri wenu kwa faida ya wanachi. Nyie ndio tunaowategemea.

    ReplyDelete
  4. Hebu sasa wataalamu ni wakati wenu wa kutoa ushauri juu ya nini kifanyike. Ni kweli nimefuatilia nimegundua kuwa zaidi ya asilimia sabini wana matatizo hayo. Anzisheni mpango wa uboreshaji afya ya meno kwa taifa. Wengi hawatambui kama hili ni tatizo.
    Eng. G.George

    ReplyDelete
  5. Unajua watu wengi tumekua tunashindwa kufuata mashrti, hata Kama umeziba jino lililotoboka na ukashindwa kulitunza ni lazima tatizo litaendelea. Kama unakua na utaratibu wa kufanya usafi kwa wataalamu wa meno Mara moja kwa mwaka, bas itakua inajulikana mapema kwamba risasa inaonyesha dalili ya kutaka kutoka na hvyo kufanyiwa marekebisho...hapa nafikir utunzaji wa jino ndo suluhisho kwakua hata kama jino limeanza kuoza kidogo likiwa linafanyiwa usafi vizuri basi halitaendekea kuoza na kuleta mdhara zaid..

    Wadau Mimi naona hili niwazo zuri sana la kuanzisha kampeni ya kitaifa ili kupunguza tatizo hili..wadau mnasemaje?

    ReplyDelete