Saturday, 31 December 2011

TUMIA MAJI KUJITIBU MAGONJWA (WATER THERAPY)

HAPPY NEW YEAR!!!!

wadau nimekutana makala ambayo imenivutia sana na ningependa niwashirikishe..

TUMIA MAJI KUJITIBU MAGONJWA (WATER THERAPY) 

Maradhi ya muda mrefu na mfupi yanayosababisha vifo, yanaweza kupona kwa njia rahisi sana.  Njia hii inaitwea “Water Therapy”  Chama cha Madaktari wa Kijapani (The Japanese Medical Association) kimetoa makala juu ya hilo na kueleza kwamba endapo mtu atatumia njia ya kujitibu kwa maji (Water Therapy” atakuwa ametibu maradhi ya muda mrefu na mfupi hususan haya yafuatayo:-
 
Kuumwa na Kishwa, Shinikiza la Damu (BP), Anaemia, Kupooza, Unene (Obesity), Mapigo ya Haraka ya Moyo na kuzimia.
Kikohozi, kuumwa na Koo (Bronchitis), Asthma na Kifua Kikuu (TB).
Hiper Acidity, Gastritis, Kuhara, kufunga choo, Piles na Kisukari (Diabetes).
Matatizo yote ya Macho.
Matatizo ya kike kubadili siku zao, Lucoria na Kansa ya Kizazi.
Magonjwa ya Pua, Masikio na Koo.
 
NAMNA YA KUTUMIA:
 
Amka asubuhi na mapema.  Kabla hujapiga mswaki na kunawa uso, kunywa maji kiasi cha bilauri nne (4).  Kisha unaweza kunawa na kupiga mswaki.  Baada ya hapo usinywe chai au kula chochote mpaka zipite dakika arobaini (40).  Baada ya kunywa chai kaa masaa mawili (2), kunywa maji bilauri nne (4),  kaa dakika arobaini (40) kabla ya kula chochote.  Baada ya kula kaa masaa mawili (2), kisha kunywa maji bilauri nne (4), kaa dakika arobaini (40) kabla ya kula chochote.  Epuka kula chakula muda mfupi kabla ya kulala.
 
Wagonjwa na watu dhaifu wanashauriwa kuanza kwa kunywa bilauri moja au mbili za maji na kuongeza kidogo kidogo m[paka kufikisha bilauri nne, na kuendelea kunywa mara kwa mara.  Kusema ukweli watu wote walio wagonjwa na wenye afya wajaribu kutumia njia hii ya kujitibu watapona na wazima wa afya hawataugua tena.
 
Kwa uzoefu na uchunguzi imebainika kwamba magonjwa mbalimbali yafuatayo yalitibiwa katika muda kama ilivyo hapa chini.
 
Ø      Shinikizo la damu (HEP)           Mwezi mmoja (1)
Ø      Matatizo ya Kujaa Gesi            Siku kumi (10)
Ø      Kisukari (Diabetes)                   Mwezi mmoja (1)
Ø      Kufunga Choo                          Siku kumi (10)
Ø      Kansa                                      Miezi sita (6)
Ø      Kifua Kikuu                             Miezi mitatu (3)
 
Wale wenye matatizo ya kujaa gesi na ugonjwa wa mifupa/baridi yabisi (Rheumatism) wanashauriwa kutumia njia hii ya Water Therapy mara tatu kwa siku kwa muda wa siku kumi (10).  Njia ya namna hii ya kujitibu ni rahisi na nyepesi sana kwa mtu na haihitaji kulipia gharama zozote.  Ni njia ya MAAJABU sana kwani inarudisha afya ya mtu bila kutumia hata dawa au fedha.  Mwanzoni mtu anaweza kujisikia kwenda haja ndiogo mara kwa mara kwa muda wa siku kama tatu lakini baadaye itakuwa kama kawaida

Thursday, 22 December 2011

MIAKA 50 NA MAENDELEO YA AFYA

Ni miaka 50 sasa tangu tanganyika ilipopata uhuru wake kutoka Kwa wakolini wa kiingereza na tangu hapo baba wa taifa akatangaza maadui watatu MARADHI, UJINGA NA UMASKINI. Baba wa taifa aliyasema hayo akiamini kabisa taifa lililoendelea linapimwa Kwa vitu hivyo vitatu, yani huduma bora za afya, uelewa mzuri Kwa wanainchi jinsi ya kujikinga na maradhi mbalimbali hii inajenga taifa lenye afya na nguvu. Taifa lisilokua na wajinga ni taifa bora zaidi kwani wasomi hutumia uwezo wao wa kielimu kubuni na na kutengeza mbinu za kuendeleza taifa na mwisho taifa lililoendelea ni taifa linye wanainchi wenye kipato kizuri cha kuwafanya waishi maisha bora.

Kutokana na jukumu la blog yetu nilikua naomba tujadili hili la MARADHI. Wakati tanganyika inapata uhuru wake(1961) kulikua na jumla ya hospitali 100, madaktari 415 na kati ya hao wazawa walikua 12 tu.

Kwa takwimu za  mwaka 2010 ratio ya daktari kwa wananchi ni 1:20408

sasa wadau Kwa takwimu hizi zinaonyesha jins taifa hili lilivyo na changamoto kubwa katika swala zima la afya haswa ikikadiriwa Kua idadi ya watanzania inakaribia milioni 45.

pamoja na matatizo yanayowakuta madaktari na manesi ni ukweli usiopingika kuwa wamefanya kazi kubwa sana katika kipindi cha miaka hii 50. WANASTAHILI PONGEZI. Je wafanyakazi hawa wanathaminiwa kutokana kazi wanayoifanyia hii nchi?

lakini sasa wadau tujiulize je? maendeleo yaliyopatikana katika sekta hii ya afya katika kipindi hiki ndio tuliyostahili au tulitakiwa kuwa zaidi ya hapa tulipo? wadau Je?  ubora na wingi wa hospitali tulizonazo unakudhi mahitaji ya watanzania? je? ni kweli elimu ya kutosha inatolewa kwa wananchi juu ya mambo ya mbalimbali ya afya.?

miaka 50 imeshapita, Je, ni nini kifanyike kupaweka sawa pale tunaposema hapoko sawa, ili ikifika miaka hamsini ijayo tusizungumze tena kuhusu matatizo tuliyoyapata kaitika kipindi cha miaka hii 50 ya mwanzo ya uhuru wetu..?

Saturday, 3 December 2011

Matatizo ya kuoza meno


Jamani wadau hembu tuulizanena Kwa kuanza kujiuliza wewe mwenyewe, hv ni Nani Kati yatu hana tatizo la meno? Fikiria ni watu wangapi(marafiki au ndugu) unaowajua kua wanamatatizo ya meno? yawezekana pia hivi karibuni hujasikia mtu akilalamika kuhusu matatizo ya meno, mdau hii haina maana Kua tatizo hili ni dogo, hili ni kubwa liko. Pengine hujasikia kwasababu watanzania tumekua na tatizo la kupuuzia maumivu madogomadogo..sasa mdau ulitaka kujua kua taizo hili ni kubwa fanya kautafiti kadogo, uliza watu 10 maswali yafuatayo;
1. umeshawahi kun'goa jino?
2. umeshawahi kupata maumivu ya jino?
3. je sasa hivi hauna jino lililooza?
Mdau majibu utakayopata yatakushangaza na utajua tatizo hili ni kubwa kiasi gani na ningependa wadau tuweke majibu yetu kwenye comments.

Wadau tatizo hili husababishwa na wadudu (germs) ambao wanapatikana katika utando mlaini na mwembamba unaojitengeneza mara Kwa Mara kuzunguka meno kutokana sanasana na vyakula tunavyokula. Wadudu hawa hutoa kemikali Kama acid na vimeng'enyo(enzyme) hivi ndio vitu vinavyofanya jino lioze,

Jinsi ya kujikinga ni kufanya vizuri usafi wameno na usafi huu upo wa aina mbili.
Njia ya Kwanza usafi wa kila siku: usafi huu hushauriwa kufanyika si chini ya Mara mbili Kwa siku yan asubuhi baada ya kuamka na usiku kabla ya kulala Inapendekezwa kufanyika hivi kwasababu ndani ya masaa 12 wale wadudu wanaoozesha meno wanakua hawajazaliana Kwa wingi kiasi cha kuleta madhara. Na unapopiga mswaki utumie dawa ya meno.

Aina ya pili ya usafi wa meno ni ile inayofanyika Mara moja Kwa mwaka, aina hii ya usafi hufanywa na wataalamu(dental specialist). Unajua mate yetu yana madini ya calcium, madini haya hulikusanya na kuganda taratibu kwenye meno na kuweka kitu kama magamba(scale) madogomadogo, sasa chini ya magamba haya wadudu hupata nafasi ya kukaa na kuzaliana, tatizo linakuja kwamba wadudu walioko maeneo haya hawawezi kuondolewa Kwa mswaki wa kawaida.
Haya ndo mambo ambayo yanaweza kutusaidia kupunguza matatizo haya ya uozaji wa meno

Wadau tuchangie chochote ambacho unahisi kinaweza kutusaidia katika kupunguza tatizo hili.

Sunday, 27 November 2011

KARIBUNI


Helooo wadau,
     Nawakaribisha sana sana katika blog yetu ya AFYA NZURI.
    
     Sasa wadau wa afya tumepata sehemu ya kutuunganisha na kutuleta pamoja, hili ni daraja la kuwaunganisha MADAKTARI WANAFUNZI, MADAKTARI, WAFAMASIA, WAUGUZI, WAFANYAKAZI WA AFYA, WAGONJWA, VIONGOZI WA KISIASA, NA WANANCHI WA KAWAIDA.

    Hapa ni mahala pa kueleza MATATIZO YETU, CHANGAMOTO, MAONI, USHAURI NA MASWALI. Wadau wote tutashiriki katika kutoa maoni, kujibu maswali na kutoa ushauri. Nia hasa ikiwa ni kuelimishana, kupeana moyo, kurekebishana, kusaidiana na kupongezana.
   
    Kwa kuyafanya hayo tunaweza kukuza uelewa wa mtu mmoja mmoja juu ya maswala mbalimbali yahusuyo afya.

    Ndugu zangu AFYA NZURI ndo msingi wakila kitu hapa duniani, mwalimu mzuri ni mwenye afya nzuri, mwanafunzi mzuri ni mwenye afya nzuri, kiongozi mzuri ni mwenye afya nzuri, mwanasyansi mzuri ni mwenye afya nzuri n.k, Afya ndo maana ya maisha.

    Wadau wote tuungane na tuboreshe afya zetu..
    BLOG itafunguliwa rasmi 04/12/2011.

 

    KARIBUNI.