Tuesday, 24 September 2013

NJIA HATARISHI ZAIDI ZA UTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA KUWAHI KURIPOTIWA

watumiaji wa madawa ya kulevya wamekua wakitumia njia mbalimbali ikiwemo KUNUSA na KUJICHOMA SINDANO.

kutokana hali ya uchumi kuwa mbaya watumiaji wamejikuta wakishirkiana vitu kama sindano, na DAMU.

uchunguzi uliofanywa na chuo kikuu cha afya cha TEXAS kikishirikiana na chuo kikuu cha tiba cha MUHIMBILI umegundua njia mbaya na hatarishi zaid kuwah kutumika, njia hizo ni FLASH BLOOD na VIPOINT

FLASH BLOOD: njia hii hufunywa kwa mtumiaji mmoja kujichoma dawa yote na bila kupita muda anavuta damu yake ambayo itakua imechanganyika na dawa kisha hyo bomba ya sindano yenye damu anapewa mtumiaji mwingine ajichume.

VIPOINT: njia hii hufanywa kwa mtumiaji mmoja kujichoma kiasi kidogo cha dawa na kubakiza nyingine kwenye bomba la sindano kisha kumpa mwingine nae ajichome.

hizi ni njia hatarishi zaidi kuwahi kutokea ambazo pia zimeripotiwa kuonekana nchini PAKISTAN. njia hizi zinasababisha maambukizi ya UKIMWI kuwa makubwa zaidi kwa watumiaji wa madawa ya kulevya.

No comments:

Post a Comment