Siku ya
Saratani Duniani mwaka 2013 (Februari 4) italenga zaidi Lengo la 5 la Azimio la
Saratani Duniani: Kuondoa mawazo potofu kuhusu Saratani,chini ya kichwa
“Saratani – Je, wajua?”Siku ya Saratani Duniani
ni nafasi ya kupaza sauti zetu kwa pamoja tukikusudia kuinua ufahamu wa
jumla kuhusu saratani na kuondoa fikra zote potofu kuhusu ugonjwa huu.
Kutoka
kwenye ngazi ya ulimwengu, ujumbe wetu utaelekezwa dhidi ya habari nne potofu
kama zilivyoainishwa hapo chini. Aidha, pamoja na kuwa kwenye mstari kwa
utetezi wa malengo ya ulimwengu, kwa pamoja tunaamini kwamba uvumi huu
unaoumiza sana unasababisha mabadiliko makubwa baina ya wanajumuiya, washirika
na wenzi kutengeneza na kujikuza katika mahitaji yao.
Uvumi 1:
Saratani ni suala la kiafya tu
Ukweli: Saratani si suala linalohusu
afya pekee. Ni suala lenye wigo mpana sana katika nyanja za kijamii, kiuchumi,
kimaendeleo na hata katika masuala yahusuyo haki za binadamu.
Uvumi 2:
Saratani ni ugonjwa wa watu wenye kipato cha juu (yaani matajiri), wazee na watu
wa nchi zilizoendelea
Ukweli: Saratani haibagui. Ni
janga la ulimwengu mzima, linaathiri watu wa rika zote, watu wa nchi zote,watu
wa kipato cha chini, cha kati na wenye
kipato kikubwa wakibeba mzigo wenye uwiano sawa.
Uvumi 3: Saratani
ni hukumu ya kifo
Ukweli: Saratani za aina nyingi
ambazo hapo awali zilidhaniwa kuwa ni hukumu ya kifo, sasa zinaweza kutibika na
watu wengi wenye saratani sasa, wanaweza kutibiwa kikamilifu.
Uvumi 4:
Saratani ndio hatima yangu
Ukweli: Saratani si hatima wala
majaliwa ya mtu yeyote, na kwa mipango kabambe, zaidi ya saratani moja kati ya
tatu zinaweza kuzuilika.
No comments:
Post a Comment