Friday, 1 February 2013

SARATANI - JE WAJUA? (2013)



Siku ya Saratani Duniani mwaka 2013 (Februari 4) italenga zaidi Lengo la 5 la Azimio la Saratani Duniani: Kuondoa mawazo potofu kuhusu Saratani,chini ya kichwa “Saratani – Je, wajua?”Siku ya Saratani Duniani  ni nafasi ya kupaza sauti zetu kwa pamoja tukikusudia kuinua ufahamu wa jumla kuhusu saratani na kuondoa fikra zote potofu kuhusu ugonjwa huu.


Kutoka kwenye ngazi ya ulimwengu, ujumbe wetu utaelekezwa dhidi ya habari nne potofu kama zilivyoainishwa hapo chini. Aidha, pamoja na kuwa kwenye mstari kwa utetezi wa malengo ya ulimwengu, kwa pamoja tunaamini kwamba uvumi huu unaoumiza sana unasababisha mabadiliko makubwa baina ya wanajumuiya, washirika na wenzi kutengeneza na kujikuza katika mahitaji yao.



Uvumi 1: Saratani ni suala la kiafya tu
Ukweli: Saratani si suala linalohusu afya pekee. Ni suala lenye wigo mpana sana katika nyanja za kijamii, kiuchumi, kimaendeleo na hata katika masuala yahusuyo haki za binadamu.

Uvumi 2: Saratani ni ugonjwa wa watu wenye kipato cha juu (yaani matajiri), wazee na watu wa nchi zilizoendelea
Ukweli: Saratani haibagui. Ni janga la ulimwengu mzima, linaathiri watu wa rika zote, watu wa nchi zote,watu wa  kipato cha chini, cha kati na wenye kipato kikubwa wakibeba mzigo wenye uwiano sawa.

Uvumi 3: Saratani ni hukumu ya kifo
Ukweli: Saratani za aina nyingi ambazo hapo awali zilidhaniwa kuwa ni hukumu ya kifo, sasa zinaweza kutibika na watu wengi wenye saratani sasa, wanaweza kutibiwa kikamilifu.

Uvumi 4: Saratani ndio hatima yangu

Ukweli: Saratani si hatima wala majaliwa ya mtu yeyote, na kwa mipango kabambe, zaidi ya saratani moja kati ya tatu zinaweza kuzuilika.