Jana wakati Niko maeneo ya chuo ninaposoma(HUBURT KAIRUKI) nilikutana na rafiki yangu Wa siku nyingi sana, baada ya maongezi mafupi aliniuliza vp mbona uko hapa unaumwa? Nikawambia hapana, kwani kila ajaye hospitali anaumwa? Akaniambia labda uwe umemleta mgonjwa au umekuja kumuona mgonjwa ua wewe ni mfanyakaz Wa humu. Kinyume na hapo lazima utakua mgonjwa.
Mtazamo alionao Huyu rafiki ni sawa na mtizamo walionao watanzania wengi sana, watu wengi tumekua tunahitaji huduma za afya pindi tusikiapo maumivu au dalili yoyote ya ugonjwa.
Watanzania hii si sawa kabisa, hospitali haziko kwaajili ya wagonjwa tu. Hata wazima tunatakiwa kuwa na utaratibu Wa kucheki afya zetu, hii husaidia sana maginjwa kugundulika katika hatua za mwanzoni kabisa na hivyo utafanya matibabu kuwa rahisi. Tujitahidi hata Kwa mwaka Mara moja.
Tuondokane na kasumba hii mbaya. Tuelimishane juu ya umuhimu Wa kufuatilia afya zetu na za watoto wetu. Tujenge taifa linalojitambua.
Hii ni kweli kabisa ndugu zangu tukiwa na tabia ya kupima afya zetu japo mara moja kwa mwaka au kila baada ya miezi sita tutakuwa tunajiweka katika hali ya usalama zaidi. Hali hii inaweza kusaidi kugundulika mapema ugonjwa kama vile Kansa katika hatua ya mwanzo na hivyo kurahisisha matibabu. Hebu tujitahidi kupima ili tuendelee kuishi kwa afya nzuri.
ReplyDeleteWashkaji vipi mbona hamchangii. Au mko bize sana na masomo au kutibu wagonjwa? Lakini mkumbuke kuwa hii ni sehemu ya kupeana hili na lile kwa ajili ya afya zetu. Ubize nao unaweza kukufanya uumwe au sio????? Ukapata ugonjwa wa msongo lazima u refresh maind kwa kupitia blogg hii.
ReplyDelete