Monday, 20 February 2012

Ni lazima tuumwe ndo tuende hospitali?

Jana wakati Niko maeneo ya chuo ninaposoma(HUBURT KAIRUKI) nilikutana na rafiki yangu Wa siku nyingi sana, baada ya maongezi mafupi aliniuliza vp mbona uko hapa unaumwa? Nikawambia hapana, kwani kila ajaye hospitali anaumwa? Akaniambia labda uwe umemleta mgonjwa au umekuja kumuona mgonjwa ua wewe ni mfanyakaz Wa humu. Kinyume na hapo lazima utakua mgonjwa.

Mtazamo alionao Huyu rafiki ni sawa na mtizamo walionao watanzania wengi sana, watu wengi tumekua tunahitaji huduma za afya pindi tusikiapo maumivu au dalili yoyote ya ugonjwa.

Watanzania hii si sawa kabisa, hospitali haziko kwaajili ya wagonjwa tu. Hata wazima tunatakiwa kuwa na utaratibu Wa kucheki afya zetu, hii husaidia sana maginjwa kugundulika katika hatua za mwanzoni kabisa na hivyo utafanya matibabu kuwa rahisi. Tujitahidi hata Kwa mwaka Mara moja.

Tuondokane na kasumba hii mbaya. Tuelimishane juu ya umuhimu Wa kufuatilia afya zetu na za watoto wetu. Tujenge taifa linalojitambua.